Simba kuendeleza msako wa pointi tatu hadi ubingwa VPL

Kikosi chetu leo kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kucheza na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ikiwa na lengo moja tu la kusaka alama tatu hadi tutakapofanikiwa kutetea ubingwa wetu msimu wa 2020/21.

Hadi sasa tunaongoza ligi tukiwa na pointi …. ambapo tunahitaji alama sita tu yaani ushindi kwenye michezo miwili ili kufanikiwa kutetea ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.

Kuelekea mchezo wa leo Kocha Msaidizi, Seleman Matola amesema wachezaji wote wako kwenye hali nzuri na maandalizi yalianza baada ya kikosi kurejea jijini Dar es Salaam juzi kutoka Mwanza.

Matola amesema kuelekea mwishoni mwa msimu kila timu inahitaji kupata ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kufanikisha malengo yetu.

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu ligi inaelekea ukingoni kila timu inataka pointi tatu lakini sisi tumejipanga kushinda na lengo letu ni kupata pointi tatu katika kila mchezo hadi kutetea ubingwa wetu,” amesema Matola.

CHAMA AREJEA KIKOSINI

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amerejea kutoka nchini kwao Zambia baada ya kumaliza shughuli za mazishi ya mkewe na amejiunga na wenzake kikosini kwenye maandalizi kuelekea mchezo wa leo.

Chama amekosa mechi kadhaa lakini baada ya kurejea juzi moja kwa moja amejiunga kambini na wenzake na yupo tayari kwa mechi kama kocha atapenda kumtumia.

MANULA, TADDEO, AJIBU KUIKOSA CITY

Mlinda mlango, Aishi Manula na kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga watakosekana kwenye mchezo wa leo kutokana na kuitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu nae atakosekana kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa malaria.

MECHI YA MWISHO TULIPOKUTANA

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Desemba 13, mwaka jana tuliibuka na ushindi wa bao moja lililofungwa na Nahodha John Bocco baada ya kupokea pasi ya Clatous Chama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER