Simba kuendelea kutangaza Utalii Shirikisho Afrika

Klabu yetu itaendelea kutangaza utalii katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kama tulivyofanya msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa.

Katika mechi zetu za Kombe la Shirikisho tukianza Jumapili dhidi ya ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast wachezaji wetu watavaa jezi zilizoandikwa VISIT TANZANIA kifuani.

Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez amesema kwa sasa timu yetu inatambulika vizuri Afrika kuliko wengi wanavyodhani ndiyo maana Bodi ya Utalii imeona ni vema kuendelea kutangaza.

“Simba inaheshimika sana Afrika kuliko inavyochukuliwa hapa nchini,  Simba inaongoza kwa kuingiza mashabiki wengi Afrika hiyo ni heshima kubwa. Brand ya Simba imezidi kuwa kubwa na hii inatufanya kuendelea kutangaza utalii.

“Katika mechi zetu zote za Kombe la Shirikisho tutaavaa jezi zilizoandikwa VISIT TANZANIA kifuani kuendelea kutangaza Utalii kama ilivyokuwa msimu uliopita. Jezi mpya kwa ajili ya michuano hii zitaanza kuuzwa kesho kwenye maduka ya Vunjabei,” amesema Barbara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii, Jaji Thomas Mihayo amesema takwimu zinaonyesha idadi ya watalii wa ndani na Afrika imeongezeka kitu ambacho Simba imechangia kwa kiasi kikubwa.

“Simba ni Mabalozi wetu wa Kimataifa ndiyo maana watavaa jezi zilizoandikwa Visit Tanzania kama ilivyokuwa mwaka jana. Kupitia michezo Wananchi wameanza kuhamasika na Watanzania wamekuwa wakiongezeka katika mbuga zetu wakifuatiwa na wageni kutoka Afrika. Mchango wa Simba ni mkubwa katika Utalii,” amesema Jaji Mihayo.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER