Simba kuanza mazoezi leo

Baada ya mapumziko waliyopewa wachezaji, hatimaye leo jioni kikosi chetu kitafanya mazoezi katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena vilivyopo Bunju jijini Dar es Salaam.

Wachezaji walipewa mapumziko ya siku nne baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Juni 3 huku wale walioitwa timu zao za taifa wakiruhusiwa kwenda kujiunga nazo.

Kikosi kitakachoanza mazoezi leo kitaundwa na wachezaji ambao hawajaitwa kwenye timu za taifa na wale ambao walikuwa majeruhi na sasa wako fiti.

Mazoezi yatakuwa chini ya kocha wa viungo Adel Zrane ambaye atawarudisha katika hali ya kimichezo baada ya kutoka mapumziko.

Kikosi kinatarajia kucheza mechi kadhaa za kirafiki ingawa bado hazijafamika kabla ya ligi kurejea ambapo mchezo wetu wa kwanza utakuwa dhidi ya Polisi Tanzania, Juni 19 katika uwanja wa CCM Kirumba.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER