Simba kuanza maandalizi ya msimu mpya leo

Kikosi chetu leo kitaanza rasmi maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22 huku malengo yakiwa ni kutetea ubingwa huo wa ligi, Azam Sports Federation Cup na kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya mchezo wa fainali wa Azam Sports Federation Cup, Julai 25 wachezaji walipewa mapumziko ya muda mfupi kwenda kuziona familia zao na leo wanarejea kuanza maandalizi ya msimu mpya.

Wachezaji wote wa ndani na nje pamoja na wale wapya waliosajiliwa na benchi la ufundi wataripoti ili kuhakikisha mipango inakwenda kama ilivyopangwa.

Baada ya wachezaji kuripoti leo, kesho kikosi kitaingia kambini moja kwa moja kuanza maandalizi ya msimu.

Timu inajiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayoanza kati Septemba 10-12 kabla ya kuanza mshike mshike wa ligi kuu Septemba mwishoni.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. The coming season shall be even harder than the previous one, So our preparation should reveal the kind difficulties ahead of us!!! Discipline, motivation and determination will take us higher …..!! Sumba 4ever

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER