Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limeitaja Simba kuwa miongoni mwa timu 10 ambazo hazitaanza hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
CAF imeweka wazi majina ya timu 54 ambazo zitashiriki michuano hiyo msimu huu huku timu yetu ikiwa miongoni mwa zile ambazo zitaanza hatua ya kwanza.
Hii ni mara ya kwanza kwetu kuanzia hatua ya kwanza kutokana na mafanikio tuliyopata msimu uliopita kwa kufanikiwa kufika robo fainali ya michuano hiyo.
Timu nyingine ambazo hazitacheza hatua ya awali ni Wydad Casablanca, Raja Casablanca, Zamelek, Al Ahly, ES Tunis, Esente Setif, Horoya, Mamelod na TP Mazembe.
One Response
Nawapongeza team yangu ya simba kwa usajiri mzuri sana wenye marengo ya kuwa na team nzuri na kubwa hapo baadae