Simba kimataifa zaidi, yazindua App

Klabu yetu leo imezindua rasmi App ambayo itarahisisha wanachama, wapenzi na mashabiki kupata taarifa za moja kwa moja kuhusu kila kitu kinachoendelea ndani ya timu.

Appy hiyo itawawezesha wanachama na wapenzi ambao watakuwa mbali na uwanja au nje ya nchi kuona kila kinachoendelea kama mahojiano ya moja kwa moja na kocha pamoja na wachezaji kabla na baada ya mechi.

Baada ya kuipakua App hii ambayo itapatikana kupitia Android na IOS gharama yake kwa mwezi itakuwa Sh 2,000 pekee.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ezekiel Kamwaga amewataka wapenzi na mashabiki kupakua App hiyo kwa kuwa kiasi cha pesa kitakachopatikana kitaingia moja kwa moja katika uendeshaji wa timu kama gharama za kambi na usajili.

“Kama kila Mwanasimba atapakua App na kila mwezi atakuwa analipia Sh 2,000 atakuwa anaichangia klabu yake moja kwa moja na mafanikio yanayopatikana anakuwa ameshiriki,” amesema Kamwaga.

Kamwaga amesema kuelekea mchezo wa kirafiki utakaopigwa leo usiku dhidi ya Olimpique Club Khouribga nchini Morocco kikosi kitakachocheza, matokeo pamoja na mahojiano ya mwalimu yataanza kuwekwa kwenye App.

Kamwaga ameongeza kuwa tarehe rasmi ya kilele cha Tamasha kubwa la Simba Day itatangazwa saa mbili usiku kupitia App.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER