Simba kamili kuivaa Yanga kesho

Kikosi chetu leo kimefanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuivaa Yanga kesho katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni.

Mazoezi hayo yamefanyika katika viwanja vyetu vya Mo Simba Arena saa sita mchana ambapo benchi la ufundi chini ya Didier Gomes limeweka wazi kuwa kila kitu kipo sawa.

Kikosi kipo tayari na wachezaji wamepanga kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi na kuchukua Ngao ya Jamii.

Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison ndiye pekee aliyekosa mazoezi kutokana na kupata maumivu ingawa pia hatakuwa sehemu ya mchezo kutokana na kufungiwa mechi tatu.

Kama tutafanikiwa kuifunga Yanga kesho na kutwaa Ngao ya Jamii itakuwa ni mara ya tano mfululizo na kuweka rekodi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER