Simba kamili kuivaa AS Vita kesho

Kocha Msaidizi, Seleman Matola ameweka wazi hali ya kikosi kuelekea mchezo wa kesho wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita wachezaji wote wapo tayari kwa mtanange na hakuna majeruhi.

Matola amesema morali ya wachezaji ipo juu na kila atakayepata nafasi ya kucheza kesho atakuwa tayari kuipigania nembo ya Klabu ya Simba.

Kocha Matola ameongeza kuwa anaamini mchezo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuhitaji kupata pointi tatu ili kujihakikishia kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

“Maandalizi yamekamilika wachezaji wote wapo kambini na hali zao za kiafya ziko vizuri na hakuna tutakayemkosa kuelekea mechi ya kesho.

“Tunafahamu mechi itakuwa ngumu, sisi tunahitaji alama moja kufuzu Vita inahitaji kushinda ili kufufua matumaini ya kufuzu robo fainali ila tumejipanga kushinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kundi hili,” amesema Matola.

Kuhusu kuruhusiwa kuingiza mashabiki 10,000 uwanjani Matola amesema itakuwa ni jambo jema huku akiwataka kujitokeza kwa wingi na kuwaahidi furaha kwa kupata ushindi kesho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER