Simba kamili kuanzia kesho

Wachezaji wote wa Simba waliokuwa kwenye timu mbalimbali za taifa wanatarajiwa kuanza kurejea nchini na kuingia kambini kufikia hadi kufikia kesho Alhamisi Septemba 9.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ezekiel Kamwaga, wachezaji wa Tanzania wanatarajiwa kuingia kambini jijini Arusha leo.

“Wachezaji wa Taifa Stars tayari wamemaliza majukumu katika Timu ya Taifa kwa awamu hii na wataingia kambini kujiunga na wenzao leo.

“Kuna wengine watarejea kesho lakini Taddeo Lwanga ambaye alikuwa Uganda tayari yuko nchini na ataondoka na wenzake wa Stars kwenda kambini Arusha,” amesema Kamwaga.

Wachezaji waliokuwa na timu za taifa ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Muzamiru Yasin, Kennedy Juma na Israel Mwenda wote wa Taifa Stars.

Wengine ni Meddie Kagere (Rwanda), Perfect Chikwende ( Zimbabwe), Peter Banda (Malawi) na Lwanga (Uganda).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER