Simba kambini leo kujiandaa na Coastal Union

Kikosi chetu kitaingia kambini moja kwa moja baada ya mazoezi ya leo jioni tayari kukiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ Jumapili ijayo.

Mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam saa moja usiku.

Meneja wa timu Patrick Rweyemamu, amesema wachezaji hawajapewa mapumziko baada ya mchezo wa jana kutokana na ratiba kuwa ngumu sababu za mechi kufuatana.

“Baada ya mazoezi ya leo jioni yatakayofanyika Uwanja wa Boko Veterans kikosi kitaingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi dhidi ya Coastal Union,” amesema Rweyemamu.

Tutaingia katika mchezo dhidi ya Coastal tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa bao moja tuliopata jana dhidi ya Polisi Tanzania ambao umetuongezea morali na hali ya kujiamini.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER