Simba kambini kuivutia kasi Yanga

Kikosi chetu leo kinaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao wa ligi kuu dhidi ya watani wetu wa jadi Yanga.

Mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi Jula 3, mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, inasubiriwa kwa hamu na wadau wengi wa soka ndani na nje ya nchi ambapo  inatarajiwa kuwa na msisimko hasa baada ya ile ya awali kuahirishwa.

Kikosi chetu kilianza mazoezi jana jioni kwenye viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kuelekea mchezo huo na leo kimeingia rasmi kambini.

Maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri na kila kitu kimekaa mahali pake.

Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali ipo juu lengo letu ni kuhakikisha tunatawazwa rasmi mabingwa wa ligi kwa kuifunga Yanga Jumamosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

6 Responses

  1. Naishukru sana club yangu ya simba sc kwa hatu iliyofikia nichukue nafasi kuwaomba kuanzisha program ya kutufikia wanachama Wapenzi na Mashabiki kindaki ndaki wa Simba sc ambao tupo mikoani , Mawilayani na hata katka vijiji iwepo njia ya kufungua matawi katka maeneo haya . kwa mfano mimi eneo nililopo hakuna tawi lolote la simba sc lakin tunaopenda kupata Kadi za uanachama ni wengi zaidi ya wantanzania 1500 ni washabiki na wapenzi wa Simba lakin hatujapata fursa ya kuwa wanachama.pia iwepo program ya timu baada ya ligi kuisha kucheza mechi za kirafiki mikoani na Si kubakia Dar es salaam maana Simba sc ni ya watanzania wote na wote tunaipenda kwa dhati toka mioyoni mwetu.nataman ujumbe huu ufike kwenu viongozi na muufanyie kazi.nawakilisha wansimba kutoka wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER