Simba kambini kuivutia kasi Mtibwa

Baada ya kumaliza mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, hatimaye kikosi chetu kimeingia kambini leo kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo utakapigwa Jumatano Aprili 14, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Aidha, leo wachezaji wote wameshiriki mazoezi katika Viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kabla ya kuingia kambini kujiandaa na mchezo huo.

Hadi sasa tupo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu tukiwa na alama 46 na michezo minne mkononi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER