Kikosi chetu kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC utakaopigwa Jumatano Julai 7, saa moja usiku katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Leo jioni kikosi kitaendelea na mazoezi kwenye viwanja vyetu vya Mo Simba Arena ili kuwaweka sawa wachezaji kuelekea mtanange huo.
Meneja wa timu, Patrick Rweyemamu amesema wachezaji wote wapo tayari na morali ipo juu ukizingatia matokeo yetu ya mechi iliyopita.
“Kikosi kinaendelea na mazoezi na jana kimeingia kambini tayari kujiandaa na mchezo ujao wa ligi dhidi ya KMC utakaopigwa keshokutwa,” amesema Rweyemamu.
Malengo yetu bado hayajabadilika licha ya matokeo ya mechi iliyopita ni kuhakikisha tunatetea taji letu la ubingwa kwa mara ya nne mfululizo.
3 Responses
Yes
Mm ni mpenzi na shabiki wa Simba naomba mdada jinsi ya kuwa mwanachama wa Simba. Nifanyeje!? # kila la heri katika mchezo dhidi ya KMC Inshallah tunaenda kupata point 3 zitakazofanya tuwe mabingwa
Mdada# n msaada. Typing error