Simba Day Septemba 19

Tamasha kubwa linalosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mpira ndani na nje ya nchi la Simba Day litafanyika jijini Dar es Salaam Jumapili ya Septemba 19.

Katika siku hiyo tutakitambulisha kikosi chetu kwa wanachama, wapenzi na mashabiki tutakachotumia katika msimu wa ligi 2021/22.

Kabla ya siku ya kilele Septemba 19 kutatanguliwa na wiki ambayo wanachama wetu nchi nzima watafanya shughuli za kijamii kama kuchangia damu, kutoa misaada mbalimbali, kutembelea vituo vya watoto yatima na wanaoshi katika mazingira magumu kama ilivyo ada kila mwaka.

Tamasha la Simba Day mwaka huu litakuwa ni la 13 tangu lilivyoanzishwa mwaka 2009 na limepangwa kuwa la tofauti na kimataifa zaidi kulinganisha na yote yaliyowahi kufanyika awali.

Uongozi wa klabu unaendelea kufanya mawasiliano na moja ya klabu kubwa barani Afrika ili ije kucheza nasi katika siku ya kilele katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER