Simba Day ni Agosti 3

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally ametangaza rasmi kileleni cha Simba week ambapo itafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Agosti 3.

Kwa kawaida Simba Day hufanyika Agosti 8 ya kila mwaka lakini kutokana na kuwepo kwa michuano ya Ngao ya Jamii siku hiyo tumeamua kuirudisha siku nyuma.

Ahmed amesema kabla ya kilele chake kutatanguliwa na wiki ya Simba itakayoanza Julai 26 ambayo itakuwa na matukio mbalimbali ya kijamii kama kuchangia damu, kuchangia wenye mahitaji maalum.

Ahmed amesema katika siku hiyo kutakuwa na matukio makubwa ya burudani kabla ya kuanza mchezo wenyewe ambao tutautumia kutambulisha kikosi chetu kuelekea msimu wa Ligi 2024/25.

“Sasa ni rasmi kilele cha Simba Day itakuwa Agosti 3, haitawezekana kufanyika Agosti 8 kama ilivyozoeleka kutokana na kalenda ya TFF ambayo siku hiyo tutaanza michuano ya Ngao ya Jamii.”

“Kabla ya siku ya kilele kutatanguliwa na wiki ya Simba ambayo itakuwa na matukio mbalimbali ya kijamii kama ambavyo tunafanya kila mwaka,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER