Simba, Biashara hakuna mbabe

Mechi yetu ya kwanza ya Ligi kuu dhidi ya Biashara United iliyopigwa Uwanja wa Karume mkoani Mara imemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Mchezo ulianza kwa kasi timu zote zikionekana kuhitaji bao la mapema lakini safu za ushambuliaji zikikosa umakini.

Kipindi cha kwanza tulitumia mipira mirefu na krosi za juu langoni mwa Biashara lakini ziliishia mikononi mwa mlinda mlango James Setuba.

Tulirudi kwa kasi kipindi cha pili na kuongeza mashambulizi langoni mwa Biashara lakini bahati haikuwa upande wetu.

Dakika ya 93 Nahodha John Bocco alikosa mkwaju wa penati uliopanguliwa na mlinda mlango wa Biashara, Setuba baada ya Pape Sakho kufanyiwa madhambi ndani ya 18 na mlinzi Salum Kipaga.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Shomari Kapombe, Rally Bwalya, Henock Inonga, Hassan Dilunga na Medie Kagere kuwaingiza Duncan Nyoni, Mohamed Hussein, Yusuph Mhilu, Peter Banda na Sakho.

Baada ya mchezo kikosi kinarejea jijini Mwanza na kesho kitaanza safari ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya mechi ya pili dhidi ya Dodoma Jiji itakayopigwa Oktoba 1.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER