Simba, Al Hilal hakuna mbabe

Mchezo wetu wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya Al Hilal kutoka Sudan uliopigwa Uwanja wa KMC Complex umemalizika kwa sare ya kufungana bao moja.

Tulianza mchezo kwa kasi huku tukiliandama lango la Al Hilal ingawa walikuwa imara kuzuia mashambulizi.

Mshambuliaji mpya Leonel Ateba alitupatia bao la kwanza dakika ya 26 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Ladaki Chasambi.

Kipindi cha pili tulianza kwa kasi ya kadiri huku Al Hilal wakifanya mashambulizi kadhaa langoni kwetu.

Suliman Ezzala hakuweza kuendelea na mchezo baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 53 baada ya kumchezea madhambi Augustine Okajepha.

Sergie Pokou aliisawazishia Al Hilal bao hilo dakika ya 75 kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kumzidi ujanja mlinzi Kelvin Kijili.

X1: Manula (Abel 45′), Kapombe (Kijili 45′), Nouma (Omary 88′), Karaboue (Kazi 85′), Che Malone (Hamza 45′), Kagoma (Mzamiru 60′), Chasambi (Duchu 85′), Fernandex (Okejepha 45′), Ateba (Mashaka 60′), Awesu (Mutale 69′), Kibu (Karabaka 69′)

Walioonyeshwa kadi: Ateba 16′ Okajepha 68′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER