Shikangwa apiga manne Queens ikiichakaza Alliance Girls

Mshambuliaji Jentrix Shikangwa amefunga mabao yote manne katika ushindi wa 4-0 tuliopata dhidi ya Alliance Girls uliopigwa Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.

Jentrix alifunga mabao matatu ndani ya kipindi cha kwanza huku la mwisho akitupia cha pili.

Shikangwa alifungua akaunti ya mabao kwa kufunga la kwanza dakika ya nane kabla ya kuongeza mengine dakika za 25 na 43.

Shikangwa alikamikilisha karamu ya mabao kwa kufunga bao la nne dakika ya 64.

Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi saba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER