Sebastian Nkoma kocha mpya Simba Queens

Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake ya Simba Queens, kitakuwa chini ya kocha mzoefu Sebastian Nkoma ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa.

Nkoma ambaye ana leseni A ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) anachukua nafasi ya Hababuu Ally aliyekuwa akikiongoza kikosi hicho awali.

Simba Queens ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Primier League) hivyo ujio wa Kocha Nkoma ni mipango ya uongozi kuhakikisha tunaendelea kufanya vizuri msimu huu.

Kwa nyakati tofauti Jocha Nkoma amewahi kiifundisha Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars).

Mbali na Twiga Stars, Nkoma amewahi pia kuzifundisha timu mbalimbali za Ligi kuu kama Majimaji ya Songea, Rhino Rangers ya Tabora na Moro United ya Morogoro.

Mwaka 2014 Kocha Nkoma aliiongoza Timu ya Jamhuri ya Visiwani Zanzibar katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER