Sakho Mchezaji Bora wa Mashabiki Juni

Kiungo mshambuliaji Pape Sakho amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Juni (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month baada ya kuwashinda Peter Banda na Kibu Denis.

Sakho amepata jumla ya kura 445 sawa na asilimia 58.71 akifuatiwa na Banda aliyepata kura 234 (30.87%) huku Kibu akipata kura 79 (10.42%).

Katika mwezi Juni Sakho amecheza mechi tatu kati ya tano sawa na dakika 221 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mawili.

Sakho atakabidhiwa tuzo na fedha taslimu Sh 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP kama sehemu ya zawadi hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa Sakho kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa mashabiki baada ya kufanya hivyo Januari mwaka huu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER