Sakho Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC

Kiungo wetu mshambuliaji Pape Sakho, amechaguliwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya NBC wa mwezi Juni kutokana na kiwango bora alichokionyesha.

Sakho amewashinda Idris Mbombo wa Azam FC na Shiza Kichuya wa Namungo ambao aliingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Juni Sakho amecheza mechi tatu kati ya tano tulizocheza akitumia dakika 222 na kufunga mabao matatu na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu.

Hii ni tuzo ya kwanza ya Ligi kwa Sakho huku akichukua mara mbili tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa mashabiki ya Emirateā€¦.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER