Baada ya kupona majeraha na kuwa fiti kiungo, mshambuliaji Pape Ousmane Sakho amepangwa kuongoza mashambulizi dhidi ya JKT Tanzania katika mchezo wa hatua ya tatu ya Azam Sports Federation Cup utakaopigwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.
Sakho amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili lakini leo Kocha Pablo Franco ameamua kumpanga kuongoza mashambulizi sambamba na Kibu Denis.
Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa Peter Banda na Yusuph Mhilu ambao watashambulia kutoka pembeni.
Mlinda mlango Beno Kakolanya anaanza katika mchezo wa leo akichukua nafasi ya Aishi Manula ambaye amedaka karibu mechi zote zilizopita.
Kikosi kamili kilichopangwa
Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Pascal Wawa (6), Sadio Kanoute (13), Peter Banda (11), Mzamiru Yassin (19), Kibu Denis (38), Pape Sakho (17), Yusuph Mhilu (27).
Wachezaji wa Akiba
Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Abdulsamad Kassim (25), Duncan Nyoni (23), Medie Kagere (14), Ibrahim Ajibu (10) Jimmyson Mwinuke (21).
One Response