Sakho, Banda, Kibu wachuana Tuzo Mchezaji Bora Juni

Nyota watatu wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Juni (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month).

Nyota hao ni kiungo mshambuliaji Pape Sakho, winga Peter Banda na mshambuliaji Kibu Denis ambao wameonyesha kiwango safi ndani ya mwezi Juni.

Katika mwezi Juni Sakho amecheza mechi tatu kati ya tano sawa na dakika 221 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mawili.

Kwa upande Banda amecheza mechi zote tano za sawa na dakika 342 akifunga mabao mawili.

Kibu amecheza pia mechi zote tano za ikiwa sawa na dakika 342 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana moja.

Kura zitaanza kupigwa leo saa 10 jioni kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na mwisho itakuwa Julai 2 saa sita usiku.

Mshindi atakabidhiwa tuzo na pesa taslimu Sh. 2,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

 

Unaweza kupiga kura hapa chini:

 

This poll has ended (since 2 years).
SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER