Sakho atupia tena Morocco

Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho ameendelea kuonyesha kuwa ni mchezaji hatari na hana masihara mbele ya lango baada ya kufunga bao la pekee katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Olimpique Club Khouribga uliomalizika kwa sare ya bao moja.

Sakho raia wa Senegal alitupatia bao la letu dakika ya 37 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Khouribga kabla ya kutupia mpira kambani.

Hili ni bao la pili kwa Sakho tangu ajiunge nasi ambapo pia alitupia bao moja katika sare ya mabao mawili dhidi ya FA Rabat Jumamosi iliyopita.

Khouribga walisawazisha bao hilo dakika ya 61 kupitia kwa Adama na kusababisha timu kutoshana nguvu.

Kocha Didier Gomes aliwatoa Sadio Kanoute, Sakho, Rally Bwalya, Chris Mugalu na Bernard Morrison na kuwaingiza Jonas Mkude, Abdulswamad Kassim Ally, Ibrahim Ajibu na Yusuph Mhilu.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

  1. Nawapongezen sana kwa kuweka app ya club ya simba maana hapo tutapata na kujulishana habari kuhusiana na club yetu kama wanamsimbazi “SIMBA NGUVU MOJA
    USINDI LAZIMA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER