Sakho ashinda Tuzo Goli Bora Afrika

Bao la kiungo mshambuliaji Pape Sakho alilofunga katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas, limechaguliwa kuwa bao bora la mwaka la Afrika

Sakho alifunga bao hilo Februari 13, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa acrobatic akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Shomari Kapombe.

Sakho amemshinda Zouhair El Moutaraji wa Morocco anayekipiga Wydad Casablanca ambaye aliingia naye fainali.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na gwiji wa Afrika, Jay Jay Okocha, Sakho amewashukuru wachezaji, benchi la ufundi pamoja na mashabiki waliompigia kura na kufanikisha hatua hiyo.

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa, wachezaji wenzangu, benchi la ufundi na mashabiki kwa ushirikiano walionipa mpaka kufanikiwa kuchukua tuzo hii,” amesema Sakho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER