Kiungo mshambuliaji Pape Sakho amerejea nchini Misri akitokea Rabat, Morocco kwenye hafla ya tuzo zilizotolewa juzi na Shirikisho la soka barani Afrika (CAF).
Sakho amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Misri, Dk. Emmanuel Nchimbi ambaye ampongeza kwa kushinda tuzo ya bao bora la mwaka la Afrika.
Dk. Nchimbi amemtaka Sakho aendelee kufanya vizuri kwakuwa ni mafanikio kwake kama mchezaji pamoja na timu huku akifurahi kwa kuitangaza vema Tanzania.
Baada ya kupokelewa na Balozi Dk. Nchimbi, Sakho amerejea kujiunga na wenzake kuendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi katika kambi hapa Misri.