Kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, amerejea mazoezini pamoja na wachezaji wenzake baada ya kupona jeraha la mguu lililokuwa linamsumbua.
Sakho alipata maumivu katika mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Oktoba Mosi.
Pamoja na kuanza mazoezi Sakho bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari ili kuhakikisha hajitoneshi jeraha lake.
Hata hivyo, uwezekano wa Sakho kuwepo katika kikosi kitakachocheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy Jumapili ni mdogo kutokana na kutokuwa fiti asilimia 100.