Sakho aanza kuonyesha yake Morocco

Baada ya kukamilisha usajili kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho ameanza mazoezi pamoja na wachezaji wenzake katika kambi inayoendelea nchini Morocco.

Licha ugeni kikosini Sakho ameonyesha kuanza kuzoeana haraka na wenzake kitu mbacho kinaonekana kitakuwa mchango mkubwa kwa timu.

Sakho 24, raia wa Senegal amejiunga moja kwa moja na kikosi kilichopo hapa Morocco akitokea Timu ya Teungueth FC ya nchini kwao.

Sakho ambaye anacheza winga wa kushoto amekuwa mchezaji muhimu wa Teungueth kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho msimu uliopita.

Sakho anakuwa mchezaji wa nne tuliyemsajili msimu huu baada ya Peter Banda, Yusuph Mhilu na Duncan Nyoni.

SHARE :
Facebook
Twitter

3 Responses

  1. Boresheni hii website iwe na features nyingi za habari kama vile mechi za watoto,wanawake,timu kubwa na kumbukumbu mbalimbali za mechi na historia ya simba sc

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER