Safari ya treni kwa ajili ya hamasa yafana

Safari ya treni kutoka Pugu hadi Kamata jijni Dar es Salaam katika zoezi la kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wetu wa Jumapili wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gandarmerie kutoka Niger utakaoanza saa nne usiku limefana.

Katika shughuli hiyo iliyofanyika leo asubuhi, Meneja Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amewaongoza Wanasimba kusafiri kutoka Pugu hadi Kamata kwa usafiri wa treni ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi Jumapili.

Baada ya kurejea makao makuu ya klabu Kariakoo, Ahmed ameendelea kusisitiza mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani na kushangilia mwanzo mwisho ili kuwachanganya wapinzani na hatimaye tutimize lengo la kutinga robo fainali.

“Lengo ni kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi uwanjani kuisapoti timu na kushiriki kuiwezesha kutinga robo fainali ya michuano hii mikubwa,” amesema Ahmed.

Juzi Jumatano Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu alizindua kampeni ya hamasa katika kituo cha mabasi cha Kimataifa cha John Magufuli lengo likiwa kuhakikisha mashabiki wanajitokeza kwa wingi.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER