Safari ya Queens hadi fainali

Timu yetu ya Simba Queens leo saa moja usiku itashuka katika Uwanja wa Azam Complex kucheza Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) dhidi ya SHE Corporates kutoka Uganda.

Queens ilipangwa kundi B pamoja na timu za Garde Republicaine (Djibouti), SHE Corporates (Uganda), Yei Joint Stars (Ethiopia).

Queens 6-0 Garde Republicaine

Timu yetu ilianza kutupa karata yake ya kwanza Agosti 14 kwa kucheza na Garde Republicaine ya Djibouti ambapo tuliibuka na ushindi wa mabao 6-0.

Queens 2-0 SHE Corporates

Mchezo wa pili katika hatua ya makundi ulikuwa Agosti 16 ambapo tulikutana na SHE Corporates ya Uganda na kuwafunga mabao 2-0.

Yei Joint 0-4 Queens

Mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ulikuwa dhidi ya Yei Joint Stars ya Ethiopia uliopigwa Agosti 19 ambapo tuliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mchezo wa Nusu Fainali

Nusu fainali tulikutana na AS Kigali WFC mchezo ambao ulipigwa Agosti 24 ambapo tuliibuka na ushindi mnono wa mabao 5-1.

Uwiano wa mabao

Kabla ya mchezo wa leo Queens imefunga mabao 17 na kuruhusu moja pekee. Uwiano wetu wa mabao ni 16.

Queens ikifanikiwa kushinda leo itawakilisha Afrika Mashariki na Kati katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na itakuwa timu ya kwanza Tanzania kufanya hivyo.

Kila la kheri Simba Queens! Wanasimba na Watanzania tupo nyuma yenu.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER