Sadio Kanoute ni mali ya Simba

Kiungo Sadio Kanoute (24) raia wa Mali amekuwa mchezaji wetu rasmi baada ya kumsajili kutoka Al- Ahli Benghazi ya Libya.

Akiwa Benghazi Kanoute amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza na ni moja ya sababu iliyotuvutia kumsajili.

Kanoute ambaye amecheza zaidi ya mechi 20 za Timu ya Taifa ya Mali, tunategemea mchango mkubwa kutoka kwake kutokana na uwezo wake mkubwa alio nao katika kusakata kabumbu.

Tayari kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kukaba, kushambulia, kutoa pasi za mwisho na kufunga yupo nchini Morocco na kikosi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2021/22.

Msimu ujao tumepanga kufanya vizuri hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndiyo sababu ya kusajili wachezaji wenye uwezo kama Kanoute.

Konoute anaungana na wachezaji wengine wa kigeni Peter Banda, Duncan Nyoni, Pape Ousmane Sakho na Henock Inonga ambao tayari tumewasajili.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER