Robertinho: Ushindi dhidi ya Dodoma Kesho ndiyo kipaumbele

 

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema tutaingia katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji kwa lengo la kutafuta ushindi ili kupunguza tofauti ya alama tulizoachwa na wanaongoza.

Robertinho ameongeza kuwa Simba ni timu kubwa na malengo yake ni kushinda ubingwa hivyo kila mchezo tunahitaji kupata alama tatu.

“Tuna nafasi ya kuonyesha Simba ni timu kubwa. Baada ya kambi ya wiki moja Dubai kufanikiwa tunahitaji kushinda na kuonyesha soka safi. Ili kuwa bingwa lazima kuchukua alama tatu,” amesema Robertinho.

Kuhusu wachezaji wapya tuliowasajili katika dirisha dogo lililofungwa Januari 15 Kocha Msaizidi Juma Mgunda amesema mchezaji anayesajiliwa dirisha dogo siku zote yupo tayari hana muda wa kusubiri, hata hawa tulio nao kesho tutegemee kuwaona uwanjani.

Nyota watatu ambao tumewasajili mwishoni mwa dirisha kiungo Ismael Sawadogo na washambuliaji Jean Baleke na Mohamed Mussa ni miongoni mwa wachezaji 19 tuliosafiri nao kuja Dodoma kwa ajili ya mchezo wa kesho.

Kuhusu Clatous Chama kubaki Dar es Salaam, Mgunda amesema; “Chama anasumbuliwa na mafua na Malaria yalimuanza tangu tukiwa Dubai, ndiyo maana hata mechi iliyopita alishindwa kuendelea akatolewa.

“Tumeona kwenye mitandao ya kijamii kila mtu anasema lake lakini taarifa kamili ni kwamba Chama anaumwa na amebaki Dar kuendelea na matibabu.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER