Robertinho: Tutashusha kikosi Kamili dhidi ya Singida Kesho

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate utakaopigwa Uwanja wa Liti atapanga kikosi cha kwanza ambacho kimezoeleka.

Robertinho ameweka wazi kuwa anawaamini wachezaji wake wote lakini katika mchezo wa kesho atawatumia wale wa kikosi cha kwanza kutokana na ugumu wa mchezo.

Robertinho ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na tunawaheshimu Singida kutokana na ubora walionao kwa sasa ingawa sisi ni zaidi yao na tumejipanga kuonyesha uwezo wetu.

“Nawaamini wachezaji wangu, Simba ni timu kubwa ambayo inatambulisha soka la Tanzania ulimwenguni, tunapaswa kuhakikisha tunacheza vizuri na kupata matokeo chanya.

“Mchezo wa kesho utakuwa kama ‘Derby’ Singida ni timu nzuri, tunaamini unaweza kuwa kama mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika,” amesema Robertinho.

Kwa upande wake mlinzi wa kati, Kennedy Juma amesema dakika 90 za kesho zitaamua nani ataondoka na pointi tatu ingawa kwa upande wao wachezaji wapo tayari kwa mchezo.

“Tupo tayari kwa mchezo, tunafahamu utakuwa mgumu Singida ni timu imara lakini nasi tumejiandaa vizuri na dakika 90 zitaamua,” amesema Kennedy.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER