Robertinho: Tupo tayari kwa Dodoma Jiji Kesho

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kikosi chetu kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa pili wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa kesho saa 10 jioni katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Robertinho amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo ingawa tutaendelea kukosa huduma ya wachezaji, Henock Inonga na Aubin Kramo ambao ni majeruhi.

Robertinho ameongeza kuwa kuwakosa wachezaji hao ni pengo kutokana na ubora wao lakini wengine wote wapo tayari kuipigania timu kupata ushindi.

Kama ilivyo kawaida yetu tutaingia uwanjani kwa kuwaheshimu wapinzani Dodoma lakini tumejipanga kucheza soka safi na kupata ushindi.

“Kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho. Wachezaji wapo kwenye hali nzuri kuhakikisha tunapata alama tatu. Tutaendelea kuwakosa Inonga na Kramo ambao bado ni majeruhi.

“Tunawaheshimu wapinzani Dodoma lakini tutaingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha tunacheza soka safi na kushinda,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER