Robertinho: Tunazitaka pointi tatu za Yanga Kesho

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa tutaingia kwenye mchezo wa kesho wa Derby ya Kariakoo dhidi ya watani wa jadi ya Yanga kwa lengo la kupambana kupata alama tatu.

Robertinho amesema timu kubwa siku zote lengo lake ni kuhakikisha inapata pointi tatu katika kila mchezo na hilo ndilo tumejipanga kulifanya kesho.

Robertinho amesema tunaiheshimu Yanga ni timu bora na siku zote Derby haitabiriki lakini anamatumaini makubwa na wachezaji wetu pamoja na maandalizi waliyopata.

Robertinho ameongeza kuwa amekuwa akiamini mpira wa miguu unatakiwa kucheza vizuri na kushinda na hiyo ndio falsafa yake.

“Mechi ya Derby siku zote haitabiriki. Derby inaamuliwa baada ya dakika 90 za mchezo, tunaiheshimu Yanga lakini tutaingia kwenye mchezo kwa lengo la kutafuta pointi tatu.

“Ninawaamini wachezaji wangu, wana vipaji vikubwa na tumejipanga kushinda. Sina presha ya mechi ya kesho, ni kama michezo mingine lakini kupata pointi tatu ndicho kipaumbele chetu,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER