Robertinho: Tuna muendelezo mzuri katika mechi zetu zilizopita

Kuelekea mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani Yanga utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kikosi kipo kwenye hali nzuri tayari kwa mtanange huo.

Robertinho amesema katika mechi zetu zilizopita tumekuwa kwenye kiwango bora na tumepata matokeo chanya hivyo imetuongezea morali kuelekea mchezo wa kesho.

Robertinho ameongeza kuwa ‘Derby ni Derby’ na siku zote inakuwa ngumu lakini anawaamini wachezaji wetu watafuata maelekezo ambayo wamepewa.

“Tuna muendelezo mzuri wa matokeo katika michezo yetu iliyopita, tumepata wiki moja ya maandalizi ya mchezo na wachezaji wote wapo tayari.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mechi na kucheza vizuri, nawajua vizuri wapinzani wetu Yanga tunawaheshimu lakini tumejipanga. Mpira kwangu ni sanaa napenda wachezaji wacheze na kuwafurahisha mashabiki pia,” amesema Robertinho.

Robertinho pia mewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu kwakuwa wana mchango mkubwa kwa upatikanaji wa ushindi.

“Nawapongeza sana Watanzania kwakuwa wanapenda sana mpira na wanajitokeza wengi sana uwanjani, niwaombe mashabiki wetu waje kutupa nguvu tuwalipe furaha,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER