Robertinho: Tumewasisitiza wachezaji kwenye umakini

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema benchi la ufundi limewasisitiza wachezaji kuhusu umakini katika muda wote dakika 90 kwenye mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers.

Robertinho amesema tunatakiwa kuwa makini tukiwa na mpira na tukiupoteza hii itatusaidia kupunguza makosa ambayo yanaweza kutugharimu.

Robertinho amesema katika Ligi ya Mabingwa huwa hatuangalii ushindi mnono aliyeshinda bao moja na aliyeshinda tano wote wanapata pointi tatu hilo ndilo la umuhimu.

Robertinho ameongeza kuwa tunahitaji kupata pointi tatu kesho ili kurejesha morali ya timu ingawa tunawaheshimu Vipers kutokana na ubora walio nao.

“Tunahitaji kuwa makini tukiwa na mpira na tukiupoteza, tumewasisitiza wachezaji kwenye kutumia nafasi tunazotengeneza, tunahitaji kupata pointi tatu ugenini,” amesema Robertinho.

Kwa niaba ya wachezaji, mlinzi wa kati Joash Onyango amesema tumefika Uganda tukiwa tunajua mchezo utakuwa mgumu, Vipers ni timu bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu.

“Vipers ni timu nzuri, tunaiheshimu lakini tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunashinda na kuchukua alama zote tatu ugenini,” amesema Onyango.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER