Robertinho: Tumewafunga Ihefu Juzi, Kesho ni mechi mpya

Licha ya ushindi mnono wa mabao 5-1 tuliopata dhidi ya Ihefu FC juzi katika mchezo wa Robo Fainali wa Azam Sports Federation Cup, Kocha Mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kesho haitakuwa mechi rahisi.

Robertinho amesema katika mpira kila mchezo ni historia mpya na una mipango yake hivyo tumejipanga kucheza dakika 90 mpya katika Uwanja wa Highland Estate.

Robertinho ameongeza kuwa Simba ni timu kubwa na lengo lake ni moja kucheza vizuri na kushinda mechi.

“Ni kweli tumewafunga juzi lakini hii ni mechi nyingine, kuna dakika 90 mpya za kuthibitisha ubora uwanjani.

“Hata wao wataipitia mechi iliyopita kuona makosa waliyofanya na kujipanga upya nasi tumejipanga kutumia mbinu zetu kuhakikisha tunapata pointi tatu,” amesema Robertinho.

Robertinho ameendelea kuwaomba mashabiki kujitojeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu kwakuwa mchango wao ni mkubwa kusaidia kupatikana kwa ushindi.

“Mashabiki ni muhimu na uwepo wao  uwanjani una msaada mkubwa kwa mashabiki, nawaomba na kesho waje kwa wingi,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER