Robertinho: Tumejipanga kucheza vizuri na kupata ushindi

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema katika mechi zetu tatu za ligi zilizosalia tumejiandaa kucheza vizuri na kupata ushindi mnono.

Robertinho amesema Simba ni timu kubwa inapaswa kucheza vizuri kila mchezo bila kujalisha matokeo ya mechi iliyopita.

Robertinho ameongeza kuwa malengo yetu yaliyobaki sasa ni kuhakikisha tunamaliza msimu kwa kushinda mechi zote zilizobaki ili kuwapa furaha mashabiki wetu na itatupa hamasa kuelekea msimu mpya wa ligi.

“Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa, bila kujalisha kimetokea nini tunapaswa kuhakikisha tunashinda mechi tatu zilizosalia.”

“Jana nimeongea na wachezaji wangu kuhusu michezo hii iliyobaki na tupo tayari kuhakikisha tunashinda ili kuwapa furaha mashabiki wetu,” amesema Robertinho.

Akizungumzia mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting Robertinho amesema utakuwa mgumu lakini tupo tayari kupambana kuhakikisha tunashinda.

 

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER