Robertinho: Sina presha na mchezo wa kesho

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa hana presha yoyote kuelekea mchezo wa kesho wa ufunguzi wa michuano ya African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly licha ya kukiri itakuwa mechi ngumu.

Robertinho amesema kuwa tunaiheshimu Al Ahly kwakuwa ni timu kubwa na ina uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini Simba pia ni kubwa na ipo tayari kwa mchezo wa kesho.

Robertinho ameongeza kuwa pamoja na ubora na uzoefu walionao Al Ahly barani Afrika lakini mpira ni sasa hivyo tupo tayari kwa dakika 90 za kesho kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

“Sina presha na mchezo wa kesho licha yakuwa ni mkubwa, hata mimi nikiwa mchezaji kule Brazil nimewahi kukutana na mechi kama hizi kwahiyo naifurahia na sina presha.”

“Ni kweli tunacheza mechi kubwa, Al Ahly ni timu bora na ina uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini mpira ni sasa na tupo tayari kwa dakika 90 za kesho,” amesema Robertinho.

Akizungumzia kuhusu kurejea kwa mlinzi wa kati, Henock Inonga ambaye alikuwa majeruhi Robertinho amesema “Henock ni mchezaji bora barani Afrika urejeo wake utatuongezea nguvu na nategemea kumtumia kwenye mchezo wa kesho.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER