Robertinho: Simba ijayo itakuwa imara zaidi

Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema baada ya muda wa miezi minne aliyokaa na timu anaamini katika siku za baadae tutakuwa na kikosi imara.

Robertinho amesema timu yetu inacheza kwa maelewano mazuri ikiwa na mpira hata isipokuwa nao na hilo ni jambo jema kwenye soka.

Ingawa tumepoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Raja Casablanca usiku wa kuamkia leo kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, Robertinho amewapongeza wachezaji kwa mchezo mzuri.

“Nina muda wa miezi minne hapa lakini hii timu itakuwa imara zaidi siku chache zijazo. Timu inacheza vizuri ikiwa na mpira na hata isipokuwa nao.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kucheza vizuri ingawa tumepoteza kwa mabao matatu, ilikuwa mechi nzuri Raja ni timu bora,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER