Robertinho, Ntibazonkiza waibuka kideda NBCPL Mei

Kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amechaguliwa kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC wa Mwezi Mei.

Robertinho amewashinda Melis Medo wa Dodoma Jiji na Daniel Cadena wa Azam FC ambao alikuwa ameingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

Robertinho ametuwezesha kuahinda mechi tatu za Mwezi Mei ambazo zilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting, Polisi Tanzania, Coastal Union na sare moja dhidi ya Namungo FC.

Kwa upande wake Said Ntibazonkiza amechaguliwa mchezaji bora wa Mwezi Mei wa Ligi Kuu ya NBC.

Katika mwezi Mei, Ntibazonkiza amefunga mabao saba na kusaidia kupatikana kwa mengine mawili.

Ntibazonkiza amewashinda Prince Dube wa Azam FC na Charles Ilamfia ya Mtibwa Sugar aliokuwa wameingia nao fainali ya kinyang’anyiro hicho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER