Robertinho: Ni furaha kucheza vizuri na kupata ushindi mnono

Kocha Mkuu Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amefurahishwa na kiwango tulicho onyesha katika ushindi wa mabao 3-0 tuliopata dhidi ya Ruvu Shooting.

Robertinho amesema ni jambo jema kucheza soka safi na kupata ushindi mnono sababu inaongeza furaha kwa mashabiki.

Robertinho pia amesema aina yake ya ushangiliaji katika mabao ya leo alikuwa anajaribu kuwapa furaha mashabiki waliojitokeza.

“Nimefurahia ushindi wa leo kwa sababu mbili, kwanza tumecheza vizuri halafu pia tumepata mabao mengi, hilo ndilo kubwa.”

“Kuhusu nilivyokuwa nashangilia nilikuwa nawafurahisha mashabiki ambao walikuwa wakiniambia nicheze,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER