Robertinho: Lengo letu ni moja tu kufuzu Robo Fainali Mabingwa Afrika

Kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi kuwa lengo ni moja kupata ushindi katika mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya ili kutinga robo fainali.

Robertinho amesema haitakuwa mechi rahisi kutokana na ubora wa wapinzani na tunawaheshimu Horoya lakini tumejiandaa vizuri kimwili na kiakili kuhakikisha tunapata ushindi.

Robertinho ameongeza kuwa anawaamini wachezaji wake na wao wanamuamini pia hivyo anaona ushirikiano uliopo utaleta tija na utakuwa siraha nzito kuelekea mchezo wa kesho.

“Lengo letu ni moja kushinda na kuingia robo fainali, tunawaheshimu wapinzani wetu Horoya lakini tumejiandaa kikamilifu kuhakikisha tunashinda.

“Nawaamini wachezaji wangu, tumeweza kushinda mechi mbili nyumbani na ugenini dhidi ya Vipers na tumecheza vizuri pia hata kesho tutafanya hivyo siku zote mimi ni mtu chanya,” amesema Robertinho.

Robertinho ameendelea kusema “tutakuwa mbele ya mashabiki wetu ambao mara zote wapo nasi kutupa sapoti.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER