Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kesho ni siku muhimu na kubwa kwa Wanasimba wote sababu wanasubiri kwa hamu kuiona timu yao kwa ajili ya msimu wa mashindano 2023/24.
Robertinho amesema tuna kikosi bora ambacho Wanasimba wenyewe watafurahi kukiona kesho kwenye Simba Day.
Robertinho ameweka wazi kuwa yeye ni muumini wa kucheza soka safi kutokana na asili yake hivyo hata kesho kwenye mchezo dhidi ya Power Dynamos anategemea hicho ndicho kitakachotokea.
Robertinho ameongeza kuwa Power Dynamos itakuwa kipimo kizuri kuelekea michuano ya ndani pamoja na kimataifa kwakuwa ni timu bora ambayo ni mabingwa wa Zambia.
“Kesho ni siku muhimu kwa Wanasimba wote, wanataka kuja kuiona timu yao. Na niwahakikishie tuna tima imara msimu huu.
“Tuna mashindano mengi msimu huu, mchezo dhidi ya Power Dynamos utakuwa kipimo kizuri kwetu,” amesema Robertinho.