Robertinho: Haikuwa rahisi kupata pointi tatu Liti

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ameweka wazi mchezo dhidi ya Singida Fountain Gate ulikuwa mgumu, haikuwa rahisi kuondoka na alama zote tatu katika Uwanja wa Liti.

Robertinho amesema Singida ni timu imara na inacheza kwa malengo lakini imekutana na timu bora leo.

Robertinho amewapongeza wachezaji kwa kuhakikisha wanapambana kwa hali yoyote na kufanikisha kupatikana kwa alama tatu ugenini.

Robertinho ameongeza kuwa malengo yalikuwa kupata alama sita ugenini kwenye mechi zetu mbili zilizopita na hilo limefanikiwa ingawa haikuwa rahisi.

“Ilikuwa mechi ngumu, Singida ni timu imara na ilitupa upinzani mkubwa lakini Simba ni kubwa zaidi na tumeonyesha hilo kwa vitendo.

“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi nzuri waliyofanya, nawapongeza pia mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kuja kutupa sapoti wamechangia pakubwa ushindi huu,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER