Robertinho: Haikuwa rahisi kuifunga Ihefu

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahia ushindi wa mabao 2-1 tuliopata dhidi ya Ihefu kutokana na mchezo kuwa mgumu.

Robertinho amesema ratiba imekuwa ngumu sababu tunapata muda mfupi wa kujiandaa kabla ya mechi kutokana na ratiba kubana lakini kikubwa pointi tatu zimepatikana.

Robertinho ameongeza kuwa katika mchezo wa leo ilibidi kuwapumzisha Kibu Denis na Jean Baleke katika dakika 45 ili kuwandaa kwa ajili ya mchezo unaofuata wa Derby.

“Ratiba ni ngumu, tumetoka kushiriki michuano mikubwa ya African Football League (AFL) na tumefanya mazoezi siku mbili kabla ya leo kushuka uwanjani.

“Ndio maana nawapongeza wachezaji wangu, haikuwa kazi rahisi lakini kikubwa tumepata pointi tatu muhimu nyumbani,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER