Robertinho, Baleke wakabidhiwa tuzo zao za NBC

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ na mshambuliaji Jean Baleke wamekabidhiwa tuzo zao za Ligi Kuu ya NBC za Mwezi Machi.

Robertinho amechaguliwa kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi uliopita baada ya kuwashinda Nasreddine Al Nabi wa Yanga na Abdallah Mohamed ‘Baresi’wa Tanzania Prisons.

Kwa upande wa Baleke amewashinda Daruweshi Saliboko wa KMC na Jeremia Juma wa Tanzania Prisons.

Wawili hao wamekabidhiwa tuzo maalum kutoka Bodi ya Ligi, mfano wa hundi ya Sh. 1,000,000 pamoja na Kisimbuzi cha Azam TV.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER