Robertinho awasifu wachezaji ushindi dhidi ya Ihefu

Kocha mkuu, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amewasifu wachezaji kwa kuonyesha kiwango safi katika ushindi wa mabao 5-1 tuliopata dhidi ya Ihefu FC uliotufanya kuingia Nusu Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC).

Robertinho amesema wachezaji walikuwa makini kuhakikisha tunatumia kila nafasi tunayopata hali iliyopelekea kuimaliza mechi kipindi cha kwanza.

Robertinho amesema katika mchezo wa leo amewapumzisha baadhi ya wachezaji kwakuwa tuna ratiba ngumu mwezi huu kwahiyo tunatakiwa kuipa umuhimu kila mechi.

“Tumecheza vizuri, tumepata mabao mengi na tumeingia nusu fainali hilo ni jambo zuri. Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi nzuri waliyofanya.

“Baada ya kupata mabao manne kipindi cha kwanza ilibidi niwapumzishe baadhi ya wachezaji na kuwaingiza vijana sababu tuna ratiba ngumu iliyo mbele yetu,” amesema Robertinho.

Robertinho amewashukuru pia mashabiki waliojitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuisapoti timu na mara zote wamekuwa wakifanya hivyo.

“Nawashukuru mashabiki kwa kuja kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu, wanachangia kiasi kikubwa matokeo yanayopatikana uwanjani,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER