Robertinho awapongeza wachezaji sare ya Azam

Licha ya kutoka sare ya bao moja dhidi ya Azam FC kocha mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amewapongeza wachezaji kwa kupambana kutafuta alama tatu ingawa hatukufanikiwa.

Robertinho amesema tumecheza vizuri lakini bao la mapema kipindi cha kwanza lilitufanya kutoka kwenye mfumo uliotufanya kupoteza nafasi.

Robertinho amesema kipindi cha pili alibadili mfumo wa kuwaingiza washambuliaji watatu wenye kasi ili kuwafungua Azam ambao mara nyingi walikuwa nyuma mpaka tukafanikiwa kusawazisha.

“Kwanza nawapongeza wachezaji wangu, wamejitahidi kupambana kutafuta ushindi. Tulitamani kupata pointi zote tatu lakini lazima tukubali tulichojaaliwa na huu ndio mpira.

“Baada ya kuruhusu bao la mapema kipindi cha pili tulibadili mfumo na kutumia washambuliaji watatu ili kuongeza presha na kuwafanya Azam kufanya makosa.

“Tulimuingiza Jean Baleke, Habib Kyombo na Kibu Denis na kuwatoa Pape Sakho, Saido Ntibazonkiza na John Bocco ambao waliongeza kasi na tulibadili hali ya upepo na kupata bao la kusawazisha,” amesema Robertinho.

Robertinho amewapongeza mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu ingawa hatujapata matokeo ya kufurahisha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER